| NOEL EN
SWAHILI !!!
|
|
|
NOELI NJEMA: LEO WOKOVU INAINGIA KATIKA NYUMBA YETU
24.12.2008 Par P. Luigi
HamJambo wandugu, kaka na dada, ya Kongo yetu. Amani ya bwana wetu Yesu Kristu iwe pamoja nanyi wote, pale mulipokaa. Ningetamani sana kuona sura yenu. Kusikia sauti, na zaidi na zaidi kuambatana nayi kwa siku kuu hii ya Noeli ili tuweze kusali na kufikiri pamoja na tuweze pia kutupatiana matakio mema ya Noeli ya salama, Noeli ya undugu, Noeli njema.. Tunakutana leo kwa kusikia pamoja Neno la Mwenyezi Mungu, ndiyo Neno la uzima wetu.
1.KUSIKIA
Ndiyo Enjili ya siku ya leo: Luka 2,1-14
1Siku zile Kaisari Augusto, mtawala wa milki ya Kirumi, aliamuru ya kwamba watu wote wa milki yake waandikishwe. 2Hii ilikuwa ni sensa ya kwanza kufanyika nayo ilitokea wakati Kirenio alipokuwa liwali wa Siria. 3Watu wote walikwenda katika sehemu walikozaliwa ili waandikishwe huko. 4Yusufu alitoka mji wa Nazareti uliopo Galilaya akaenda mpaka Bethlehemu mji wa Daudi kwa sababu yeye alikuwa wa ukoo wa Daudi. 5Alikwenda huko kujiandikisha pamoja na mchumba wake Mariamu ambaye kwa wakati huu alikuwa mja mzito.
6Walipokuwa Bethlehemu, wakati wa Mariamu kujifungua uli fika, 7naye akamzaa mtoto wa kiume, kifungua mimba. Akamfunika kwa vinguo na kumlaza horini, kwa sababu hapakuwa na nafasi katika nyumba ya wageni.
8Usiku ule walikuwako wachungaji wakilinda kondoo zao nje ya mji. 9Ghafla malaika wa Bwana akawatokea, na utukufu wa Mungu ukawang'azia pande zote. Wakajawa na hofu kuu. 10Lakini malaika akawatuliza akisema: ``Msiogope! Nawaletea habari njema ya furaha kubwa, na habari hii ni kwa faida ya watu wote! 11Kwa maana leo katika mji wa Bethlehemu, amezaliwa Mwokozi ambaye ndiye Kristo Bwana. 12Na hivi ndivyo mtakavyomtambua: mtamkuta mtoto mchanga amefunikwa vinguo na kulazwa horini.''
13Mara jeshi kubwa la malaika wa mbinguni likatokea na pamoja wakamsifu Mungu wakiimba: 14``Atukuzwe Mungu juu mbin guni, na duniani iwepo amani kwa watu ambao amependezwa nao.''
15Malaika hao waliporudi mbinguni wale wachungaji walish auriana: ``Jamani, twendeni Bethlehemu tukaone mambo haya ya ajabu yaliyotokea, ambayo Bwana ametufahamisha.''
16Kwa hiyo wakaenda haraka Bethlehemu, wakawakuta Mariamu na Yusufu; na yule mtoto mchanga alikuwa amelala mahali pa kulia ng'ombe. 17Walipomwona mtoto, wakawaeleza yale waliyokuwa wameambiwa. 18Na wote waliosikia habari hizi wakastaajabia yale waliyoambiwa na wachungaji. 19Lakini Mariamu akayaweka mambo haya yote moyoni mwake, akayafikiria mara kwa mara.
20Wale wachungaji wakarudi, huku wakimtukuza Mungu na kum sifu kwa yale waliyoyasikia na kuyaona.
2.Kufikiri
Leo ni siku kuu ya Noeli. Siku ya matakio. Siku ya uwema. Siku ya undugu. Sisi wakristu wakatolika tunakumbuka siku ya kuzaliwa kwake pangoni mwa Betlehemu Yesu Kristu, Mwana wa Mungu, Mwokozi wetu. Ndiyo alama kwenu, mtakuta mtoto mchanga.
Noeli ya Mwaka huu inatukuta namna gani? Na hali gani nchini? Na hali gani jamaani mwetu? Na hali gani rohoni mwetu? Masito mengi inaendelea kabisa kututia katika woga na misukusuku ya kila haina. Watu wengi walisha kupoteza matumaini yote, wanaona tu kama maisha yaho ilisha kuwa ya mateso mengi mno.
Wengi walipita jimboni mwetu kuhubiri na kutangaza wokovu wa bure. Bila Mungu hatuwezi kitu, na hakuna jambo lisilowezekana kwa Mungu Mwenyezi. Giza ni mingi kandokando yetu, na mara na mara rohoni mwetu.
•Mungu anasema: “Wale wote waliokuwa katika giza leo wanaona mwangaza na wanaokoa” . Ni mwangaza ya Noeli, mwangaza yenyi kutoka katika pango ya Betlehemu. Yule mtoto atasema siku moja: “ ukitaka kuwa namwangaza, unifwate, kwani ni miye mwangaza wa dunia”.
•Luka anatuambia katika enjili ya Noeli: “nawapasha habari njema, na muwe na furaha tele: leo Mwokozi anazaliwa kwenu.” Tunaweza kurudia katika njia ya matumaini? Ndiyo, leo tunaweza, kwani Noeli anawambia wakongomani wote na kwa mara ingine: “ musiogope, musimame, kwani wokovu wenu haiko mbali”. Ni kweli mtoto huyo ni Emanueli: Mungu pamoja nasi.
•Na Luka, katika enjli anaendelea kusema: “ Endeni Betlhemu… Mutakuta…” Inatufaa kusimama. Inatufaa kuacha hali yetu mbaya. Hali gani? Hali ya wivu, ya ukali wa vita , ya uwongo, ya kuiba mali ya serkali na mali za watu, ya kuua, ya kuangusha chini hoja na heshima ya watu, ya ukabila, na kazalika. Tunaweza kuendeshha daftari yetu, lakini sisi wote tunajua kama maovu ni mengi kati yetu. Na tunajua pia kama maovu yote yanatokea kwa chemchem moja: ndiyo uyanguyangu na kiburi chetu.
•Yoane anasema: “neno alijifanya mtu, lakini watu walio wake hawakumpokea…” Hatuwezi kupokea mwangaza kama tunaendela kupenda giza. Hatuwezi kupokea amani ya nchi kama sisi wenyewe hatupendi kutupa silaha yetu. Silaha hawezi kuokoa nchi yetu!
•“ Sifa kwa Mungu mungu mbinguni, amani duniani kwa watu wa mapenzi mema” wanaendela kuimba malaika mbinguni usiku huu. Turudie kwa Mungu. Tujinyenekee mbele ya mtoto huyu. Na tujifunze kabisa. Yeye wokovu wa dunia anafika kwetu bila silaha, bila askari, bila uwezo, bila unguvu. Nawambia kwa wakubwa wote wa nchi, wale wenye uwezo kama vile Kabila, Assemblée Générale, MONUC, etc. , kwa wale wenye kuitiwa “Wabwana wa vita” kama vile Nkunda, Kagame, Museveni : Leo Noeli , muwe na mapenzi mema, murudishe amani kwetu, na mutupe zana za vita, nguvu za kijeshi, silaha zote za jeshi.
3.KUSALI
Ee mtoto Yesu, unachukua kuzaliwa hapa kwetu na namna isio ya kawaida: pango ya nyama, malazi ya majani, ubaridi wa usiku kati. Lakini ni mambo ya maajabu sana ili dunia waone wazi kama Mungu wetu anajinyenyekeza kwa kuwasimisha watu wote. Kutoka pangoni mwangaza yako inaangara ku dunia mzima ili watu waone njia ya salama, ya uhuru, ya usawa, ya undugu. Aksanti, ee mtoto Yesu, aksanti sana.
Noeli njema kwa wote na mwaka mpya ya heri. Mungu Mwenyezi atubarikie, atulinde, atukinge. Kwa heri.
© kakaluigi 2008
|
Notre espérance n'est pas encore morte. Par
P. Luigi
Sifa kwa Mungu
mbinguni, na amani duniani kwa watu wa mapenzi mema..
Oui il y a pas de choses qui ne marchent pas bien. Trop de mal qui
règne dans grand Congo, et nous sommes tous pleins de doutes que toute
cette souffrance finira un bon jour. Feu Munzihirwa me disait : « Ca
ira, ça ira… » Mais jusqu'à quand ? « Ca ira, ça ira… »
L'espérance de Noel, d'un enfant qui dans une mangeoire est le Sauveur
du Monde. L'espérance d'un Messie, différents des autres messies
venus de part tout dans le monde qui nous ont fait des grandes
promesses. L'espérance de Nairobi, pour croire à un monde de paix dans
nos régions. L'espérance d'une guerre qui peut avoir son mot définitif
, celui de la fin. L'espérance de voir nos enfants congolais et
congolaises sortir d'un cauchemar terrible.
L'espérance d'un peuple au
bout de son souffle.
Noel est là en ce 2008 pour nous dire que tout est possible.
Noël, c'est Dieu qui vient à la rencontre des hommes.
Noël c'est Dieu qui devient petit pour que les petits deviennent grands.
Noel c'est l'Emmanuel, Dieu avec nous qui veut faire de nos petites
histoires des histoires saintes de salut.
Noël, c'est l'amour, la fraternité, la tolérance, la solidarité
Noël c'est penser à tous ces enfants qui meurent pour la faim, pour la
maladie, par manque d'argent-
Jésus Christ est né a Bethleem pour nous dire tout cela. Il est né
dans la pauvreté dans une grotte.
Sont les pasteurs qui recevaient le message: "Je vous annonce une
grande joie, Aujourd'hui dans la ville de David, Bethleem est né le
Sauveur du Monde." Aujourd'hui sont les hommes de toute race et nation
le même annonce est dit dans toutes les langues: Sifa kwa Mungu
mbinguni, na amani duniani kwa watu wa mapenzi mema...
Joyeux Noel 2008
Pere
Luigi est congolais de coeur du Grand Kivu. Il a vecu pres
de 40 ans au Congo, son pays d'adoption. Ses paroissiens,
ses amis, ses freres et soeurs congolais l'appellent
affectuesusement "Kakaluigi". Sur Congonet
Radio, il vous parle chaque dimanche de l'Evangile
et de son pays: la RDC. Kakaluigi est actuellement en
sejour en Italie.
Contact:
kakaluigi@gmail.com
|